HabariNews

Mawaziri wateule kikaangoni bunge likianza zoezi la kuwapiga msasa

Bunge la kitaifa leo limeanza rasmi zoezi la kuwapiga msasa Mawaziri walioteuliwa na Rais William Ruto kufuatia kufutiliwa mbali kwa baraza la awali kutokana na shiinikizo ya vijana wa GEN-Z.

Katika orodha ya mazairi walioratibiwa kuhojiwa alhamisi hii ya 1 Agosti, 2024 ni waziri mteule wa Usalama na masuala ya ndani Profesa Kithure Kindiki, Dakt. Deborah Barasa wa afya, Alice Wahome wa ardhi, Julius Ogamba wa Elimu na Soipan Tuya wa Ulinzi.

Akijibu maswali ya wabunge, waziri mteule Profesa Kindiki amepata wakati mgumu kueleza uwezo wake wa kusimamia wizara hiyo muhimu hasa baada ya matukio ya ukiukaji wa katiba ikiwemo utekaji nyara, maafisa wa polisi kuwakabilia waandamanaji hasa waliopinga mswada wa fedha 2024 na maandamano ya azimio ambayo yalipelekea zaidi ya watu 70 kuaga dunia 2023.

Prof. Kindiki ambaye itakuwa ni mara yake ya pili kukaguliwa na Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Nyadhfa baada ya kuhudumu katika baraza la kwanza, alisema yeye ndio mtu sahihi wa kutatua masuala ya usalama nchini.

“ I believe I’m suitable for reappointment because, during those 21 months in office I have been able to keep the country fairly safe, especially in the fight against terror and also the crime of banditry has reduced by more than 75%,” Kindiki aliambia wabunge.

Kadhalika Kindiki alieleza kamati hiyo ya wabunge inayoendesha zoezi hilo la kupiga msasa mawaziri wateule kwamba Mamlaka huru ya kutathmini utandakazi wa polisi nchini IPOA inafaa kupewa nafasi kuwachunguza maafisa wa usalama wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi.

Aidha akijibu swali kuhusu visa vya utekaji nyara raia vilivyoshuhudiwa wakati wa maandamano ya vijana wa Gen Z mwaka huu 2024, Kindiki alisema wakati alipokuwa waziri wa kitaifa alitoa mwelekeo kwa idara za usalama kuwa serikali haikubaliani na visa vya utekaji.

Alisisitiza kwamba visa hivyo vinafaa kuangaziwa kwa umakini na na hatua mwafaka za kukomeshwa zichukuliwe.

“During my tenure as minister, I made it clearly to the police that abductions, extra-judicial killings and extra-constitutional means of apprehending offenders, is against government polisy, is against the constitution and is against international law.” Alieleza.

Katika ziara zake za ndani ya nchi baada ya kulazimika kukaa ikulu kwa takriban mwezi mmoja, rais William Ruto alitembelea kaunti ya Tharaka Nithi nyumbani kwa Kindiki mnamo Alhamisi 25 Julai, 2024.

Ni katika ziara hiyo ambao rais Ruto alimpigia debe Kindiki baada ya kumteua tena kushikilia wizara hiyo kwa mara nyingine takriban wiki 2 hivi baada ya kumfuta kazi.

Ruto akimtaja Kindiki kama waziri aliyeelewa majukumu yake ifaavyo na sasa wabunge wanajukumu moja tu waidhinishe uteuzi huo au kuukata.

Ikumbukwe kuwa katika maandamano ya GEN-Z yaliyodumu kwa zaidi ya wiki tatu, vijana hao walitaka baraza lote livunjwe na mawaziri wote wasirudishwa katika baraza jipya la mawaziri.

Zoezi hilo kuwahoji mawaziri wateule 20 linatarajiwa kutamatika kufikia Jumapili 4 Agosti, 2024.

BY MAHMOOD MWANDUKA