HabariNews

Baraza kuu la Kitaifa la Chama cha UDA limetengua uteuzi wa Katibu Mkuu Cleophas Malala

Katika taarifa iliyotolewa hii leo muda mchache uliopita Kamati hiyo imesema kwamba Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Hassan Omar Hassan atakuwa na kushikilia nafasi ya Katibu Mkuu kwa Muda.

Kamati hiyo aidha imeagiza kwamba Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ifanye marekebisho yanayohitajika na kuendelea na awamu ya kwanza ya Uchaguzi wa Mashinani katika Kaunti nyengine ambazo hazijafanya Uchaguzi wake.

Hapo awali, Mkanganyiko ulitikisa Chama hicho baada ya Mwenyekiti wake Cecily Mbarire ambaye ni Gavana wa Embu kuitisha kikao cha Baraza kuu hii leo, Katibu Mkuu Cleophas Malala aliyeondolewa, alikimbilia Mahakamani kusitisha Mkutano huo akitaka agizo la muda mbele ya Jaji wa Mahakama ya Juu Lawrence Mugambi aliyesisitiza Mkutano huo utafanyika Ijumaa Juma lijalo ya tarehe 9.

BY NEWS DESK