Uncategorized

Waziri Mkuu wa Bangladesh Ajiuzulu na Kutoroka Nchi

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina ameripotiwa kujiuzulu na kukimbia nchi kutokana na maandamano yanayoendelea ya kupinga uongozi wake.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la habari la Al Jazeera pamoja na vyombo vya habari nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo amepanda helikopta ya kijeshi, msaidizi aliiambia Al Jazeera, baada ya umati wa watu kupuuza amri ya kutotoka nje ya kitaifa kuvamia ikulu ya waziri mkuu huko Dhaka.

Mapema siku ya Jumatatu (Agosti 5), maelfu ya waandamaji walilivamia kasri la Waziri Mkuu huyo baada ya duru kufahamisha kuwa ameikimbia nchi kufuatia maandamano makubwa ya kumshikiza ajiuzulu.

Kituo cha televisheni cha Chanel 24 kilionesha picha za makundi ya waandamanaji wakikimbilia kuingia ndani ya makaazi ya waziri mkuu huyo katika mji mkuu Dhaka, huku wakizipungia mikono kamera wakati wakisherehekea.

Matangazo ya vituo vya televisheni vya Bangladesh yaliwaonesha waandamanaji wakivamia kasri la Hasina, kuzipindua samani, kuvunja milango na kuchukuwa vitanda na vitu vingine wakiwemo kuku walio hai.

Takriban watu 300 wamefariki kutokana na maandamano ya wiki kadhaa ambayo mamlaka yametaka kukandamiza.

Kufuatia usiku wa ghasia mbaya zilizosababisha vifo vya takriban watu 100 siku ya Jumapili, hali ya wasiwasi ilikuwa imesalia siku ya Jumatatu.

Kufikia alasiri saa za eneo hilo, hata hivyo, vyombo vya habari viliripoti kwamba hali ya barabarani ilikuwa imegeuka kuwa sherehe baada ya habari za kuondoka kwa Hasina kuenea.

BY NEWSDESK