HabariNewsSiasa

Odinga Afichua Rais Mstaafu Uhuru Alimtaka Aongee na Rais Ruto Kutuliza Hali Tete Nchini

Kinara wa Azimio la Umoja Raila Odinga amefichua kuwa rais mstaafu Uhuru Kenyatta alimwomba azungumze na rais William Ruto ili kutatua mzozo uliosababishwa na maandamano ya Gen Z.

Akizungumza huko kaunti ya Elgeyo Marakwet, Raila amesema Uhuru alimwambia azungumze na Ruto kwa sababu taifa lilikuwa linaelekea kusambaratika hasa baada ya kufikisdhwa ukingoni na maandamano ya vijana hao.

Sasa saa ile nchini inachomeka Uhuru ndio alinipigia mimi simu, akanambia mimi tafuta bwana Ruto uongee na yeye Kenya ikichomeka hatutakuwa na nchi nyingine, mpaka tuzime hii moto watu waketi chini waelewanie. William akanitafuta na mimi niliongea nay eye wazi.” Akasema.

Odinga amesema kutokana na wasiwasi na matakwa yaliyoibuliwa na wakenya alikubali kushiriki kusaidia kuunda serikali Jumuishi ya msingi mpana ili kuokoa nchi na wala si serikali ya muungano.

Na unajua mimi sifichi mambo nasema direct, magazeti hao wanandika Raila na Ruto ati handsheki, hakuna handshake hakuna, mimi niliongea na Ruto wakenya wameudhika na ndio tumeona hawa vijana wamejitokeza.

Nilimwambia hawa watu wako umeweka pale hawajafanya kazi vile inahitajika ndio maana imekuwa hivi.” Akasema

Wakati uo huo Odinga amesema kuwa matakwa na mamalamishi ya vijana wa Gen Z yalikwua halali na mwafaka kushinikiza uongozi sahihi, na kwamba kilio chao si ya kupuuzwa kamwe.

By Mjomba Rashid