HabariLifestyleNewsSiasa

Jimmi Wanjigi Kulala Seli; akamatwa baada ya Kujiwasilisha katika Afisi za DCI

Mfanyabiashara mashuhuri na mwanasiasa Jimmy Wanjigi atalazimika kulala kwenye kituo cha polisi cha Kamukunji, Nairobi baada ya kushikwa na maafisa wa upelelezi kwa tuhuma ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Wanjigi ambaye amehojiwa takribani kwa saa nne katika makao makuu ya polisi ya Nairobi Area ameshikwa alipojilasimisha baada ya kuwindwa na polisi kwa muda na hata wiki jana kusakwa nyumbani kwake siku mbili pasi mafanikio.

Wakili wake John Khaminwa anasema hatua hiyo ni kinyume cha sheria ikizingatiwa kwamba tayari kulikuwa na agizo la mahakama, linazuia polisi kumnasa.

Kinachofanyika ni kudharauliwa sana, hivi sivyo haki inapaswa kufanyika kweli. Wamemkamata wamemuweka kizuizini sasa wanampeleka kituo cha Kamkunji na kesho asubuhi atafikishwa mahakamani.” Alisema Khaminwa

Maafisa wa Polisi wanaamini kwamba Kinara huyo wa chama cha Safina ambaye amekuwa mpinzani mkali wa serikali ya Kenya Kwanza kwa kiwango kikubwa alihusika pia katika kufadhili maandamano ya vijana, maandamano ambayo yalitatiza serikali kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.

Kushikwa kwake akiwa na mawikili John Khaminwa na Willis Otieno pamoja na familia kumezua wasiwasi hasa baada ya mahakama kumlinda dhidi ya polisi.

Baadhi ya wafuasi wake wakiwemo kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Eugen Wamalwa wa DAP-K walifika katika kituo cha Kamukunji anakozuiliwa baada ya kukamatwa kwake.

Kwa sasa haijulikani kama atawachiliwa huru baadaye ama atafunguliwa mashtaka na kufikishwa mahakamani Jumanne, lakini kinachosadikika kwa sasa ni kuwa atakuwa mgeni wa serikali hadi.

By Mjomba Rashid