HabariNews

Mshukiwa Mkuu wa Mauaji ya Kware avunja Seli na Kutoroka na washukiwa wengine

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Kware, Embakassi jijini Nairobi ametoroka kituoni alikokuwa akizuiliwa.

Collins Jumaisi Khalusha mshukiwa wa mauaji ya takriban wanawake 42 ametoroka katika kituo cha Polisi cha Gigiri alikokuwa akizuiliwa pamoja na washukiwa wengine 12 raia wa Eritrea.

Kulingana na ripoti ya polisi mshukiwa huyo mkuu ametoroka kizuizini pamoja na raia hao 12 waliokuwa wakizuiliwa kituoni hapo kwa kosa la uhamiaji haramu.

Inaripotiwa kuwa mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ya leo afisa wa polisi aliyekuwa akisimamia kituo hicho Konstebo Gerald Mutuku aligundua hilo alipokuwa ametembelea seli hiyo akiwa na meneja wa mgahawa kuwapa kiamshakinywa washukiwa hao.

Maafisa wa polisi wamesema wameanzisha uchunguzi wa kusaka maeneo waliko washukiwa hao.

Itakumbukwa kuwa Khalusha amekuwa akizuiliwa akisubiri kufikishwa kortini kusikiliza kesi dhidi ya mauaji ya wanawake 42 waliokutwa katika jaa la Kware mtaani Embakasi.

Khalusha ambaye aligonga vichwa vya habari mwezi uliopita baada ya kukiri kuwaua wanawake 42 na kisha kuitupa miili yaoalidai kuwa mhasiriwa wake wa kwanza alikuwa mkewe Imelda ambaye alimnyonga hadi kufa na kumkatakata kabla ya kuyatupa mabaki ya mwili wake kwenye jaa la taka eneo hilo.

Hata hivyo mshukiwa huyo baadaye alidai kuwa polisi walimtesa na kumlazimisha akiri kutekeleza mauaji hayo yanliyoripotiwa kufanyika katika kipindi cha kati yam waka 2022 na Julai 11 mwaka huu.

By Mjomba Rashid