HabariNewsUncategorized

Mashirika ya utetezi wa haki yashinikiza haki ya ajira za nyumbani

Mashirika mbali mbali ya utetezi wa haki yanashiniza serikali kuangazia upatikanaji wa haki hasa kwa wafanyakazi ambao wamekuwa wakikosa malipo hasa wanaofanya kazi za nyumbani.

Evalyne Atieno kutoka shirika La utetezi wa wanawake FIDA, alisema wafanyakazi wengi wa nyumbani wamekosa kufahamu haki zinazowalinda na wamekuwa wakipitia dhulma katika utendakazi wao.

Bi Atieno aliongeza kuwa shirika hilo limekuwa likiwasaidia wafanyakazi hao katika utatuzi wa kesi wanazopitia chini ya waajiri wao akisistiza haja ya hamasa kuhusu haki kwa wajiri na waajiriwa.

Serikali inatakikana ijuwe kuwa hapa nchini Kenya tuko na wale wafanyakazi ambao hawalipwi na wanapaswa kufuata katiba inasema vipi kwa wale wafanyakazi ambao hawalipwi na inastahili wapate haki zao vipi ili wasiweze kudhulumiwa, Kama Fida tumekuwa tukiwasaidia katika ushauri wa kisheria kama wanataka na pia kuwawakilisha kisheria kupitia mradi wetu wa legal representation na self-representation ili waweze kupata haki zao kortini”, alisema Evalyne.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha kutetea Maslahi ya Wafanyakazi Kudheiha-Khamisi Juma Mkhoka allsema wafanyakazi wengi wamekuwa wakipitia madhila kutokana na kukosa miungano ya kuwatetea.

Alishinikiza waajiri kuhakikisha wanaweka mikakati bora ya makubaliano kati yao na wanaowaajiri ikiwepo kutia saini mkataba ili kusaidia wakati kunapotokea tatizo.

“Kila Mfanyakazi anahaki ya kujiunga na chama chochote cha kutetea haki zao na vile vile pia katika hizi sheria za leba inatuambia kunauhuru wa muajiri na muajiriwa kukaa chini na kukubanilana mishahara yao na kuja na mkataba wa makubaliano utakaowaelekeza katika kazi ambayo wanafanya, kwa hivyo mfanyakazi wa nyumbani anahaki zake na ziko ndani ya sheria na ikiwa muajiri ataenda kinyume na sheria ofisi za leba ziko wazi yakwamba huyu mfanyakazi wa nyumbani atatetewa haki zake na yule mwajiri amlipe”, alisema Juma Mkhoka

Wakizungumza katika kongamano lililoandaliwa na shirika la Youth Alive Kenya-chini ya mradi wa Time to care jijini Mombasa Afisa wa mipangio katika shirika hilo Rahma Issa, alisistiza haja ya mashirika ya kijamii kuzingatia hamasa ya usawa na haki kwa waajiriwa wote.

“Leo tumeweza kuzungumza maswala kadha wa kadha tukiwa na waajiri wa care workers pamoja na care workers, tumeweza kudadisi ni jinsi gani tunaweza kuja pamoja kufanya kazi na haya mashirika ili kuhakikisha hata tukifanya kazi pale nyumbani tunaweza kusimama katika sheria na haki, kama Youth alive tunaamini hatuwezi kufanya kazi pekeyetu,na tuna mashirika kadha ambayo tunafanya kazi nayo, na huu mradi wa time to care tunafanya kazi na Kudheiha na Oxfam Kenya na tunaangalia ni vipi maswala ya unpaid care na paid care yanaweza kutekelezwa pale nyumbani”, alisema Rahma Issa.

Naibu Chifu eneo la Frere town eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa Hilaria Fara, alisema idadi kubwa ya wafanyakazi za nyumzani wamekuwa wakipitia dhulma mbali mbali.

“we do referrals pia kukiwa kuna kesi zozote za changamoto kati ya mwajiri na mwajiriwa tunajaribu kuingilia kati hasa maswala ya malipo, na ikiwa itashindikana sana tunawaelekeza kwa mashirika mengine, kiwango kikubwa ni wale ambao hawalipwi, wale wanaofanya kazi za nyumbani mara nyingi ndio changamoto tunazopata nyanjani, mana kwa sasa kuna mtindo wa wale wamama wa kufua wanakuja pengine kwa wiki mara mbili, saa nyengine wanakandamizwa kwa zile kazi wanazofanya, kwa hivyo jukumu langu mimi kama chifu pale chini nikuhamashisha manake tumekuja kutambua wananchi wengi hawajui haki zao”, alisema Hilaria Fara, Naibu Chifu eneo la Frere town.

By Joseph Jira