HabariNews

KUPPET Yasitisha Mgomo na Kuagiza Walimu wao Kurejea Shuleni

CHAMA cha walimu wa shule za sekondari na vyuo vya kadri nchini, KUPPET hatimaye kimesitisha mgomo wa walimu wanachama wake ulioanza wiki jana na kuwaagiza warejee shuleni.

Hii ni baada ya maafisa wakuu wake kukutana na mwajiri wao TSC jijini Nairobi na kuafiki kuusitisha mgomo huo uliodumu kwa wiki nzima.

Katika kikao cha pamoja na wanahabari baada ya mkutano wa kutwa nzima, Katibu Mkuu wa KUPPET, Akelo Misori na Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC Nancy Macharia wamewaambiwa wanahabari kuwa mgomo huo umesitishwa kwa sasa huku wakisubiri masuala ambayo yangali yatashughulikiwa na TSC.

Misori aidha amebaini kuwa walimu walioshiriki mgomo hata hivyo hawatachukuliwa hatua yoyote.

BY MJOMBA RASHID