HabariNews

Shule ya Upili ya Wasichana ya Ng’ombeni iliyoko Chonyi eneobunge la Kilifi Kusini imefungwa kwa muda

Shule ya Upili ya Wasichana ya Ng’ombeni iliyoko Chonyi eneobunge la Kilifi Kusini imefungwa kwa muda, wanafunzi wakilazimika kurejea nyumbani.

Hii ni baada ya bweni la shule hiyo kuteketea moto usiku wa Jumanne na kupelekea zaidi ya wanafunzi 160 kukosa malazi.

Uamuzi wa kuifunga shule hiyo umejiri baada ya mkutano wa bodi wa shule hiyo kuafiki hatua hiyo, kutokana na wanafunzi wengi kupoteza malazi, mavazi yao na bidhaa zao nyingine.

Moto huo umeripotiwa kuanza mwendo wa saa mbili usiku wa Jumanne wanafunzi walipokuwa madarasani kwa.

Naibu mwalimu Mkuu wa Shule Monico Joseph amesema wanafunzi wote wako salama.

By News Desk