HabariLifestyleNews

Serikali Yatoa Hakikisho la Kuimarisha Usalama Kaunti ya Lamu

Serikali imeapa kuendeleza mikakati kabambe ya kuimarisha usalama kaunti ya Lamu dhidi ya ongezeko la visa vya ugaidi.

Akizungumza huko Mpeketoni katika ibada ya mazishi ya Naibu gavana wa Lamu Raphael Munyua, Naibu Rais Rigathi Gachagua ametoa hakikisho kuwa serikali ya Kenya kwanza umeleta idara zote za kiusalama kuwakikishia wakazi wanaishi kwa amani na usalama.

Gachagua amesisitiza umuhimu wa jamii kuishi kwa amani, upendo na kuzingatia usalama katika eneo hilo ambalo lina vivutio vya kitalii kwa ajili ya maendeleo na ustawi.

Lazima wananchi wa Lamu walindwe kwa hali na mali, na ndiyo Serikali imeweka askari na raslimali nyingi sana hapa kuhakikisha kwamba watu wa Lamu wanapata amani na kila mtu anapata nafasi ya kufanya kazi yake sawasawa na kila mtu anaishi bila wasiwasi, na ndio serikali imejitolea na tulitoa hakikisho kama serikali kwa hilo Rais, mimi na wengine serikalini wamejitolea kuhakikisha watu wa Lamu wanaishi kwa amani.” Akasema.

Akijibu suala la Seneta mteule wa Lamu Shakila Abdalla aliyesisitiza kuondolewa kwa mbwa wa kunusa mizigo ya abiria katika vizuizi vya ukaguz barabarani kwa kutokuwa sahihi kwa waislamu, Gachagua amsesma kuondolewa kwa umbwa hao itakuwa ni kuvuruga mikakati ya kiusalama.

Amesisitiza kuwa mbwa hao wa kunusa wanafanya kazi nzuri kwa kusaidia maafisa hao kukagua mizigo na kutambua vilipuzi na hakuna njia mbadala inayowekza kutumika kwa sasa.

Viongozi wengine walioandamana na Naibu rais ni Gavana wa Lamu Issa Timami na mwenzake wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir, Seneta wa Lamu Joseph Githuku, mwakilishi wa akina mama Monicah Marubu, manaibu gavana wa Tana River, Mombasa na Kilifi, wabunge miongoni mwa wengine.

By Mjomba Rashid