HabariNews

Ndugu Wawili na Mwanaharakati waliotoweka Wapatikana wakiwa Hai kaunti ya Kiambu

Ndugu wawili na Mwanaharakati waliopotea eneo la Kitengela mnamo Agosti 19, wakati wa maandamano dhidi ya Serikali hatimaye wamepatikana katika Kaunti ya Kiambu.

Kulingana na Rais wa chama cha mawakili LSK, Faith Odhiambo, ndugu hao Jamil na Aslam Longton wamepatikana wametupwa eneo la Gachie Kaunti ya Kiambu.

 “Nimearifiwa  kuwa mili ya Jamil na Aslam imepatikana eneo la Gachie mapaka wa kiambu na Nairobi,tunashukuru kwa maombi kweli yamesaidia, tunashukuru Mungu kwa kuwa wako salama.” alisema kupitia mtandao wa x.

Hatahivyo mwanaharakati Bob Njagi amepatikana hai eneo la Tigoi Kaunti ya Kiambu, baada ya baba yake mzazi Longman Njagi kuaarifu kuwa yu salama salmin.

Nimepigiwa usiku wa manane na maafisa wa Tigoni police station na kuniarifu kuwa kijana wangu amepatikana hai.” Amesema Mzee Njagi.

“Njagi amechukuliwa na ndugu yake wa kiume katika police station. Tunashukuru Mungu kwa habari nzuri tumekua tukiomba, tunashukuru.”

Habari hizzi zilitolewa saa chache baada ya Inspekta Jenerali mpya wa Polisi Douglas Kanja kusema kuwa Idara kuu ya polisi (NPS) haikuwa ikiwazuia watatu hao.

By News Desk