HabariNews

Gavana wa Kericho Aponea shoka la Kubanduliwa Afisini

Gavana wa Kericho Dkt. Eric Mutai ameponea shoka la kumbandua mamlakani baada ya Bunge la Seneti kuamua kusitisha vikao vya kumbandua afisini.

Maseneta 34 wamepiga kura kuunga mkono pingamizi la Gavana Mutai dhidi ya maseneta 10 waliounga mkono hoja ya kumbandua iendelee kusikilizwa.

Huyu hapa Spika wa Seneti Amason Jeffa Kingi amkisoma uamuzi baada ya bunge hilo kupiga kura kuhusiana na hoja hiyo.

Gavana huyo wa Kericho alikuwa amewasilisha pingamizi kuzuia Seneti kujadili hoja hiyo akisema kuwa Bunge la Kaunti ya Kericho lilishindwa kufikia kiwango cha thuluthi mbili kufikia uamuzi wa kumbandua afisini.

Hoja ya kumbandua afisini Gavana Mutai iliwasilishwa katika bunge la Kaunti ya Kericho na mwakilishi Wadi wa Sigowet, Kiprotich Rogony.

Walimstumu Gavana Mutai kwa ukiukaji wa katiba, utumizi mbaya wa ofisi na ubadhirifu wa raslimali za umma.

By Mjomba Rashid