HabariNews

Polisi Wawanasa Washukiwa Sugu wa Uhalifu wa Mapanga Kiembeni, Mombasa

Maafisa wa Polisi kaunti ya Mombasa wamewanasa washukiwa 8 wa uhalifu katika mtaa wa Kiembeni eneobunge la Kisauni.

Kulingana na kamanda wa Polisi kaunti ya Mombasa Peter Kimani, wanane hao ni miongoni mwa wahalifu sugu ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi maeneo mbalimbali mjini Mombasa.

Kimani amebaini kuwa washukiwa hao wa umri kati ya miaka 14-22 wametiwa mbaroni katika oparesheni ya usiku wa kuamkia Alhamisi, polisi wakiwanasa na mapanga manane, runinga na simu kadhaa; sasa wakisubiri kufikishwa mahakanani kufunguliwa mashtaka.

Miongoni mwa washukiwa hao ni mshukiwa mkuu wa kisa cha kukatwa mkono mwanabodaboda mmoja kilichofanyika mwezi mmoja uliopita.

Kamanda huyo wa polisi amewashukuru raia wanaoendelea kushirikiana na idara ya usalama kufichua uhalifu kwa kupiga ripoti huku akitoa onyo kali kwa wanaoshiriki uhalifu kwamba watakabiliwa vilivyo kisheria.

By Mjomba Rashid