Raia wa kigeni aliuawa mapema alasiri ya Alhamisi baada ya kugongwa na msafara wa rais uliokuwa ukienda kwa kasi katika barabara ya Ngong jijini Nairobi.
Kisa hicho kimetokea karibu na eneo la Adams Arcade wakati msafara huo ulikuwa ukisafiri kutoka Lang’ata na kuelekea eneo bunge la Kibra.
Mwathiriwa huyo anayetajwa kuwa ni mzungu mwenye umri wa makamo, aliripotiwa kugongwa alipokuwa akijaribu kuvuka barabara hiyo yenye shughuli nyingi, akionekana kutofahamu magari yanayokuja.
Afisa mkuu anayefahamu tukio hilo amelitaja tkio hilo kuwa ajali mbaya na tukio la kuhuzunisha.
Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City, ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
By Mjomba Rashid