HabariNews

Robert Prevost Mzaliwa wa Marekani Achaguliwa Papa Mpya

Kadinali Robert Prevost wa Marekani amechaguliwa kuwa papa mpya na kiongozi wa Kanisa Katoliki la Roma siku ya Alhamisi.

Prevost amechukua jina la Papa Leo wa (14) kuwa kadinali mwandamizi aliyetangazwa kwa umati wa watu katika uwanja wa St. Peters Square.

Prevost, mwenye umri wa miaka 69, kutoka Chicago, Illinois, ndiye papa wa kwanza kabisa kutoka Marekani na atajulikana kama Leo XIV (Papa Leo wa 14).

Hadi kuchaguliwa kwake alikuwa akihudumu kama mkuu wa Dicastery wa kanisa kwa Maaskofu na ametumia muda wake mwingi akitumikia nchini Peru, na ana uraia wa Marekani na Peru.

Maelfu ya mahujaji na watazamaji wenye udadisi katika uwanja wa St Peter’s walishangilia na kupiga makofi huku moshi ukionekana na kengele kuanza kulia, kuashiria kuwa taasisi hiyo yenye umri wa miaka 2,000 ina papa wake wa 267.

Kabla ya kutangazwa, majina kadhaa yalikuwa yanatajwa kumrithi Papa Francis kuongoza Kanisa Katoliki.

 By News Desk