HabariNews

Kenya Kwanza kutumia sheria ya fedha ya 2022 ya serikali ya Jubilee

Wachanganuzi wa masuala ya sheria na uongozi nchini wanasema huenda serikali ya Kenya Kwanza kapata wakati mgumu zaidi baada ya mahakama Kuu kuamua kuwa sheria ya fedha ya 2023 ni haramu na kinyume cha katiba.

Wakili Dancan Okatch alieleza kwamba baada ya mahakama kutoa uamuzi wa kuibatilisha sheria hiyo serikali imefungwa mikono kuitumia kukusanya ushuru.

Hii ni licha ya sheria ya fedha ya mwaka 2024 kupata pingamizi na hatimaye kutupiliwa mbali na rais William Ruto.

Wakili Okatch akieleza kwamba iwapo serikali itaridhia uamuzi wa mahakama, haina budi kutumia sheria ya fedha ya mwaka 2022 ya serikali ya Jubilee.

Kulingana mtaalamu huyo ajenda ya Kenya kwanza na Jubilee ni tofauti na hivyo kutumia sheria hiyo ya fedha itawia vigumu serikali ya sasa kutekeleza shughuli na hata kutimiza ahadi kochokocho ilizotoa kwa Wakenya.

Hata hivyo, Okatch alibaini kwamba kuna ngazi moja tu iliyosalia ya kukata rufaa katika mahakama ya upeo.

“At this point the government has no option because taxes must continue to be collected. So the government must revert noow to the 2022 Finance Act, which in my view may not be within the actual parameters or agenda of the Kenya Kwanza administration” alieleza wakili Okatch.

Hata hivyo wakili huyo alibaini kwamba mahakama ilikuwa na nafasi ya kuagiza serikali kurudisha ushuru uliokusanywa kupitia kwa sheria hiyo jambo ambalo mahakama ilishindwa kulibaini kwa madai kwamba halikuwa suala kuu katika kesi hiyo kwenye Mahakama Kuu.

“Actually, the Court of Appeal, fell short of saying that they ought to refund the taxes that they have collected. Only that it said, that was not an issue at the High Court,” alisema Okatch.

Awali baada ya Mahakama ya rufaa kutoa uamuzi huo wa kesi iliyokuwa imewasilishwa na Mwanaharakati aliye seneta wa Busia Okiah Omutata alishabikia ushindi katika kesi hiyo.

Omutata na watu wengine waliowasilisha kesi hiyo, alisema sheria hiyo imeongeza gharama ya maisha na kumhujumu mwananchi wa kawaida.

Hata hivyo Licha ya uamuzi huu kuiacha serikali katika njia panda, hasa baada ya kutupiliwa mbali mswada wa fedha wa mwaka 2024, baadhi ya wabunge wakiongozwa na kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichungwa walikosoa na kupinga uamuzi huo wakisisitiza kuwa kwa shughuli za serikali zitalemaa zaidi.

“ When I read that judgement this afternoon Honourable Speaker I was left wondering and asking myself, does it mean then, that all acts parliament passed by this house post 2010 anality in law and unconstitutional..?” Alihoji Ichungwa.

BY MAHMOOD MWANDUKA