HabariLifestyleNews

Bei ya Mafuta Kusalia Zilivyo Kulingana na Tangazo jipya la EPRA

Bei ya mafuta ya Petroli, Dizeli na mafuta ya taa itasalia jinsi ilivyo kwa kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Mamlaka ya Kudhibiti Kawi na Petroli nchini Kenya (EPRA) imetangaza bei za mafuta kuanzia leo tarehe 15 Agosti 2024 hadi Septemba 14, 2024.

Bei za mafuta zimesalia bila kubadilika katika tangazo jipya la bei za bidhaa hiyo muhimu.

Mafuta ya petroli yatauzwa kwa Sh. 188.84 kwa lita, dizeli Sh171.60 huku mafuta taa yakiuzwa kwa Sh161.75 kwa lita jijini Nairobi kuanzia leo, Agosti 15.

Mjini Mombasa mafuta ya Petroli yatasalia kuuzwa kwa shilingi 185.66 kwa lita, Dizeli shilingi 168.48 na mafuta ya taa yakisalia kuwa shilingi 158.7 kwa lita.

Epra imesema kuwa bei hizo ni pamoja na kodi ya Ongezeko la Thamani ya asilimia 16 (VAT) kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Fedha ya 2023, Sheria ya Kodi ya Sheria ya 2020 na viwango vilivyorekebishwa vya Ushuru wa bidhaa.

By Mjomba Rashid