Baadhi wa bunge kutoka eneo la Mlima Kenya wamejitokeza kumtetea Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kupinga siasa za baadhi ya viongozi kutoka eneo hilo za kumbandua Gachagua uongozini.
Wakizungumza Mjini Mpektoni wakati wa mazishi ya aliyekuwa naibu gavana wa Lamu Raphael Munyua, viongozi hao wamesema wanaoendeleza siasa hizo wanamalengo ya kibinafsi.
“Naibu Rais hajawahi hata siku moja kusema Mlima iungane na Pwani wasiungane, wanajaribu kumdhalilisha na hatutakubali, na huyo stori ni ya jaba.”
Aidha mjadala tata wa “one man One vote One Shilling’ ukiibuka tena katika hafla ya mazishi hayo huku baadhi ya viongozi kutoka eneo la Mlima kenya wakiunga mkono mfumo wa ugavi wa mapato ya serikali kuu kwa kuzingatia idadi ya watu katika eneo, mfumo ambao umepingwa vikali na viongozi kutoka kaunti ya Lamu.
Hata hivyo Naibu RAIS aliyekuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo ya mazishi amelikwepa suala hilo na badala yake akajikita katika masuala ya amani na usalama akiwataka viongozi wote na wakenya kuzingatia amani na kusambaza siasa za kuunganisha jamii zote za humu nchini.
Wakati uo huo Gachagua amesisitiza kuwa serikali inaendeleza mikakati kuboresha usalama wa kaunti ya Lamu.
Viongozi wengine walioandamana na Naibu rais ni Gavana wa Lamu Issa Timami na mwenzake wa Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir, Seneta wa Lamu Joseph Githuku, mwakilishi wa akina mama Monicah Marubu, manaibu gavana wa Tana River, Mombasa na Kilifi, wabunge miongoni mwa wengine.
By George Oliver