Wakenya wanashauriwa kuendeleza shughuli ya upanzi wa miche na utunzaji wa mazingira katika siku hii ya kitaifa ya mapumziko kuadhimisha Siku ya Mazingira nchini.
Siku hii ya Mazingira nchini ilitenwga na serikali mwaka jana katika hatua mojawapo za kimarisha mazingira na kukabiliana na mabadilik ya tabianchi.
Waziri wa Mazingira, misitu na mabadiliko ya tabianchi Aden Duale amewasihi wakenya kujitolea na kujihusisha na shughuli ambazo zinachangia mazingira safi.
Duale ambaye anaongoza maadhimisho ya siku hii katika eneo la Hifadhi ya msitu wa Kilimani Arboretum jijini Nairobi ameitaja Siku hii kama fursa muhimu kuongeza kasi ya kuyalinda mazingira na kuongeza uhamasisho kuhusu athari za uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Siku hii ya Tarehe 10 mwezi Oktoba awali ilifahamika kama ‘Moi Dei’ kabla ya kubadilishwa kuwa ‘Siku ya Utamaduni’ na baadaye kubadilishwa tena kuwa Siku ya Mazingira baada ya Rais William Ruto kutia saini kuwa sheria mswada wa marekebisho ya ziada.
Itakumbukwa kuwa mwaka jana Rais Ruto aliongoza shughuli ya upanzi wa miti na hata kuwaagiza mawaziri wake kuzuru maeneo mbalimbali nchini kuongoza shughuli hiyo kwa lengo la kufikia azma yake ya miti bilioni 15 kufika mwaka 2032.
By Mjomba Rashid