Spika wa bunge la kaunti ya Lamu Abdukasim Ahmed amepuzilia mbali madai kuwa bunge la kaunti ya Lamu linapinga mchakato wa BBI.
Abdukasim amesema bunge la kaunti ya Lamu linaunga mkono kikamilifu mchakato wa BBI na wako tayari kuifanyia kampeni kwa wananchi ili waweze kuikubali.
Amesema wataandaa vikao na wananchi ili kuwaeleza umuhimu wa BBI badala ya kusikiza propaganda zinazoenezwa na baadhi ya watu kuhusu BBI.
Aidha amesema hawatakubali msukumo wowote wa watu kutoka nje ya kaunti hiyo kuwashawiji juu ya msimamo wao kuhusu BBI.
Amesema watu wa Lamu wako na haki ya kufanya maamuzi kwa hiari yao na wala sio kwa mapendekezo kutoka kwa watu wengine.
Comment here