HabariSiasa

Bunge la Kericho ni la 39 kupitisha mswada wa BBI

Bunge la kaunti ya Kericho ni la hivi punde kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.

Wawakilishi wadi wote katika bunge hilo wamepiga kura ya kuunga mkono kupitishwa kwa mswada huo.

Hii inafikisha 39 idadi ya mabunge ya kaunti yaliyopitisha mswada huo kufikia sasa.

Haya yanajiri huku mrengo wa Tangatanga unaohusishwa na naibu rais William Ruto ukijitokeza na kuwatahadharisha wapinzani wa kisiasa dhidi ya sherehe za mapema baada ya kaunti hizo kupiga kura ya kuidhinisha mswada huo.