HabariSiasa

Mawaziri wa kaunti sasa wataka kuongezwa mishahara na mrupurupu

Mawaziri katika serikali za kaunti sasa wanataka kuongezwa mishahara na mrupurupu, wakiitaka tume ya mishahara na malipo SRC kulizamia suala hilo kama ilivyofanya kwa kuidhinisha ruzuku ya magari kwa wawakilishi wadi.

Mawaziri hao wanasema wamesahaulika kwa muda mrefu katika suala la kutathmini mishahara na hata marupurupu.

Mwenyekiti Hezbon Onsarigo anasema mawaziri hao wanatekeleza majukumu mengi ambayo hayaambatani na mishahara wanayopata.