HabariMombasa

Kaunti ya Mombasa yatakiwa kuweka sheria thabiti kukabili uchafuzi wa mazingira

Mashirika ya kijamii yanayohusika na masuala ya mazingira hapa pwani yanaitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuweka sheria thabiti kukabili uchafuzi wa mazingira.

Afisa wa shirika la HURIA Alex Nziwi anasema ukosefu wa mpangilio thabiti kuhusu sehemu maalum za kutupa taka umechangia uchafuzi wa mazingira na kuwa changamoto kuu katika kuweka mazingira safi.

Mbali na mazingira ya kawaida Nziwi amesema kumekuwa na uchafuzi wa mazingira ya bahari kuanzia katika bandari ya Mombasa hadi eneo la Diani hatua inayohatarisha maisha ya viumbe hai baharini.

Afisa huyo amesema shughuli za kibinadamu baharini zimechangia uhaba wa samaki na kusambaratisha sekta ya uvuvi nchini.