HabariSiasa

Ruto asema changamoto kubwa inayokabili wakenya ni ukosefu wa ajira

Naibu rais William Ruto amesema kwamba changamoto kubwa inayokabili taifa hili ni ukosefu wa ajira kwa wakenya.

Akiwahutubia wananchi katika kaunti ya Transnzoia, Ruto amesema tatizo la taifa hili sio katiba kufanyiwa marekebisho bali ni kushindwa kutekeleza sheria za katiba. Wakati huo huo Ruto ameonya kuhusu siasa za makabila huku akiendelea kupuzulia mbali kauli ya rais Kenyatta

Mchakato wa kuifanyia marekebisho katiba ukiendelea kupamba moto mbunge wa Ganze Teddy Mwambire amesema serikali ya kitaifa hivi karibuni itatoa nakala za ripoti ya marekebisho ya katiba BBI kwa lugha ya Kiswahili.

Kulingana na mbunge huyo nakala hizo zitawarahishia wananchi kuelewa kwa kina ripoti hiyo kufuatia wengi wao kulalamika kwamba hawaelewi lugha ya KIINGEREZA, shughuli inayotarajiwa kuanza miezi miwili ijayo.
Wakati huo huo mbunge huyo amesema wananchi watahamaishwa kabla ya kuamua iwapo wataipitisha ripoti hiyo wakati wa kura ya maamuzi au la. Mwambire aidha amesema kilichobaki ni mswada huo kupelekwa katika bunge la kitaifa ili liweze kuujadili kabla kuandaliwa kwa kura ya maamuzi