Habari

Kesi inayomkabili aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike mbuvi Sonko imelazimika kauhirishwa baada ya sonko kukosa kufika mahakamani.

Mawakili wa Sonko wameambia mahakama kuwa mteja wano angali na maumivu na amelazwa katika Nairobi hospital akisubiri kuelekea afrika kusini kufanyiwa upasuaji.

Mawakili hao akiwepo Cicily Mila Nanyamo, wamesema mahakama ilikuwa imetoa amri ya kuzuia sonko kusafirishwa kutoka anakozuiwa.

Upande wa mashtaka umepinga madai hayo ukisema amri hiyo ilipitwa na wakati tarehe 26 mwezi februari.

Sonko anakabiliwa na mashtaka mbali mbali ikiwepo utumizi mbaya wa mamlaka na ufisadi.