HabariSiasa

RAILA akamilisha ziara yake pwani kwa kupigia debe BBI…

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amekamilisha ziara yake ya siku tano eneo la Pwani kwa kuipigia debe ripoti ya BBI katika eneo la Samburu kaunti ya Kwale.

 

Akiwahutubia wakaazi wa eneo hilo, Raila amewataka wakaazi wa Pwani kuiyunga mkono ripoti hiyo ili kutatua masuala ya mizozo ya ardhi katika eneo hilo.

 

Raila amesema kuwa suala la uswota miongoni mwa Wapwani litatatuliwa kupitia utekelezaji wa ripoti zinazofungamana na masuala ya ardhi.

 

Kwa upande wake mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed amewasuta wabunge waasi wa Kwale wanaojihusisha na mrengo wa naibu rais William Ruto.

 

Mohammed amemlaumu mbunge wa Kinango Benjamin Tayari na mwenzake wa Lungalunga Khatib Mwashetani kwa kutoshughulikia ipasavyo suala la ardhi kaunti hiyo.