Serikali ya kaunti ya Taita Taveta kupitia wizara ya afya imezindua rasmi utoaji wa chanjo ya corona, baada ya kupokea jumla ya chanjo elfu 1, 500 kutoka kwa serikali ya kitaifa.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi, Gavana Granton Samboja amesema wahudumu wa afya ndio watakaopewa kipaombele kwa sasa ikizingatiwa kwamba ndio walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa.
Hata hivyo Samboja ameirai serikali kuu kuhakikisha chanjo hio inasambazwa katika ngazi ya kaunti kwa kiwango cha juu ili wananchi waweze kufikiwa.