Wakazi wa kata ndogo ya Bofu eneo bunge la likoni kaunti ya Mombasa wanalalamikia ukosefu wa maji wakisema kwamba kuna bwenyenye anayeshirikiana na viongozi katika kusambaratisha utoaji huduma ya maji eneo hilo.
Elija ochieng mkaazi wa eneo hilo anasema kwamba kero la maji limekuwa gumzo katika eneo hilo kwa muda mrefu kiasi cha kuwa wenyeji wa eneo hilo wameachawa katika hali tata ya kutafuta maji inhali wanalipa ushuru kama wakenya wa kawaida ,
Ochieng anasema kwamba kuna bwenyenye anayeshirikiana na baadhi ya viongozi katia eneo hilo kusamabaza maji kunyume na sheria na hata kuchangia kuchanganya maji ya chumvi na maji safi ya mfereji.
Kadhalaka wenyeji hao wameshutumu vikali mwakilishi wadi wa eneo hilo la Bofu wakisema kuwa kiongozi huyo ni mwenye ubinafsi na ni mbaguaji katika utoaji huduma kwa wakazi wa eneo hilo.