Habari

Kituo kipya cha umeme chazinduliwa Kilifi.

Onyo kali imetolewa kwa wanakandarasi wanaowaunganishia umeme wakazi bila kufuata sheria.

Akitoa onyo hiyo waziri wa kawi nchini Charles Keter, amesema wanakandarasi hao watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Keter amesema kumekuwa na wanakandarasi ambao wamekuwa  na hulka ya kuchukua hongo na kuunganisha umeme kinyume cha sheria huku akiwasistiza wateja kuwatafuta wanakandarasi ambao wanaowaunganishia umeme kwa kufuata kanuni hitajika.

Wakati uo huo wakazi wa eneo hilo wameeleza kufurahiswa na mradi huo wakisema kuwa eneo hilo litaboreka na biashara kuzidi kuimarika.

Hayo yamejiri wakati wa uzinduzi wa kituo cha kusambambaza umeme katika Kijiji cha Mtondia eneo bunge la Kilifi Kaskazini kilichogharimu takribani shilingi milioni 200.