HabariSiasa

BUNGE LA TANARIVER LAPATA PIGO KUHUSU UAMUZI WA BBI,

Mahakama imefutilia mbali uamuzi wa Bunge la Kaunti ya Tana River wa kupitisha Mswada wa 2020 wa Marekebisho ya Katiba.

Katika uamuzi huo, bunge hilo halikuchukua maoni ya wananchi kabla kuupitisha mswada huo.

Hata hivyo, uamuzi huo hautaathiri mchakato wa kuifanyia katiba marekebisho kwani tayari hitaji la katiba la angalau kaunti 24 kupitishwa limeafikiwa.

Tana River ilikuwa miongoni mwa kaunti 43 zilizopitisha mswada huo unaolenga kufanyia katiba marekebisho kupitia Mpango wa BBI.

By Guracho Salad.