Habari

Visa vya wasichana kutoroshwa vyaongezeka huko Galole……

Afisa wa idara ya watoto eneo la Galole kaunti ya Tana River Maria Mboti amesema visa vya wasichana wadogo kutoroshwa na wanaume vimeongezeka na kusabisha ongezeko la ndoa za mapema eneo hilo.

Hata hivyo amesema kuna changamoto kujua idadi kamili ya wasichana hao waliotoroshwa na wanaume, akisema wengi wao hudanganya miaka hivyo kuvunja makali ya afisi hiyo kufuatilia kisheria.

Mboti amesema kuanzia kipindi cha janga la korona visa kumi pekee ndivyo vilivyoripotiwa afisini kwake huku akiongeza kwamba visa vingi haviripotiwi.

Hata hivyo afisa huyo amewahimiza wasichana kuacha tabia ya kutorokea kwa waume na badala yake watafute msingi wa maisha yao ya baadae.

Mboti amewataka wasichana wadogo kutafuta hifadhi kwa afisi za serikali mashinani wakati wowote wazazi wao wanawalazimisha kuingia kwa ndoa za mapema.