HabariKimataifa

Rais Uhuru Kenyatta hii leo atembelea makazi ya balozi wa jamuhuri ya Tanzania humu nchini

Rais akiandamana na maafisa wa ngazi ya juu serikalini kati yao wakiwa jaji mkuu Philomena Mwilu,na maspika wa mabunge yote, wote wakituma risala zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu .

Aidha Rais amemhakikishia balozi huyo kwamba kenya kwa ujumla itasimama na watu wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu na kutuma risala yake binafsi na pia kwa niaba ya wakenya kwa rais samia suluhu.

Kadhalika, spika wa bunge la kitaifa   Justin Muturi na mwenzake wa senate ken Lusaka pia wametoa rambi rambi zao kwa niaba ya bunge hizo mbili.

Balozi wa Tanzania humu nchini Dkt Stephen Simba Chaweni amemshukuru rais Uhuru Kenyata kwa   kuomboleza  na watanzania kwa utaratibu alioutoa ivi majuzi.