HabariLifestyle

KCPE KUANZA JUMATATU HUKU MATAYARISHO YAKIKAMILIKA

Kamishena wa kaunti ya Tana River Mbogai Rioba amesema mikakati imewekwa ya kuhakikisha swala la udanganyifu na wizi wa mtihani linazuiwa.

Rioba amesema maafisa wa usalama wako imara katika kila kituo cha kufanyia mitihani na sehemu za kuhifadhia mitihani ili kuzuia hali yoyote ya kutatiza mitihani hiyo.

Amesema mitihani hiyo italindwa vilivyo akidai kuna maafisa wengi zaidi ya vituo vya mitihani na kwamba swala usalama si la kutiliwa shaka.

Wakati uo huo kamishena huyo amesema katika vikao na wadau kumewekwa mfumo wa mawasiliano utakaotumika kutoa ripoti zozote zinazopania kutatiza shughuli za mtihani.

Ameongeza kuwa mikakati imewekwa kwa wanafunzi kutoka kwa jamii za wafugaji zakuhamahama na mifugo kaunti hiyo kushiriki mitihani hiyo.

Mwisho