AfyaHabari

Watu 2,008 waambukizwa corona huku 6 wakiaga dunia hii leo….

Kenya hii leo imerekodi visa vipya 2,008 vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 11,360 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 128,178.

Katika visa hivi vipya, 1,954 ni raia wa humu nchini huku 54 wakiwa raia wa kigeni, 1,090 ni wa kiume na 918 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana mwaka mmoja huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 94.

Hata hivyo watu 6 wameaga dunia kutokana na maambukizi na kufikisha idadi ya waliofariki kutokana na corona kuwa 2,098.

Jumla ya wagonjwa 1,192 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 3,777 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 124 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)