AfyaHabari

Wakaazi wa kaunti ya Machakos walalamikia ukosafu wa maji ya kunawa mikono kama njia moja ya kujikinga na maambukizi virusi vya corona…………….

Wakaazi wa kaunti ya Machakos wamelalamikia ukosafu wa maji ya kunawa mikono kama njia moja ya kujikinga na maambukizi virusi vya corona.

Aidha wakaazi hawa wamesema kuwa kuna mitungi ya maji iliyokuwa imewekwa na serikali ya kaunti wakati wa wimbi la kwanza la Corona lakini kwa sasa mitungi hiyo haina maji hali inayohatarisha afya yao.

Haya yanajiri pindi tu baada ya Rais Uhuru kutoa agizo za kufungwa kwa kaunti za Nairobi, Nakuru, Machakos, Kiambu na Kajiado.

Onyo imetolewa kwa wazazi eneo bunge la Kilifi kuwalinda watoto wao msimu huu wa likizo ndefu baada ya shule kufungwa siku chache zilizopita.

Akitoa onyo hiyo mkuu wa polisi eneo bunge la Kilifi Kasakazini Daniel Chacha amewataka wazazi kuwalinda watoto wao pamoja na kutowaruhusu kujiunga na makundi yasiyofaa.

Hata hivyo Chacha amewasihi wazazi kutenga muda wa kutosha wa kukaa na watoto wao.