HabariLifestyle

JANGA LA CORONA LAZIDI KUTIKISA SEKTA YA UTALII.

Wadau katika sekta ya Utalii hapa Pwani wanasema masharti mapya yaliyotangazwa na rais Uhuru Kenyatta ya kukabili maambukizi ya viryusi vya corona yameanza kuathiri pakubwa sekta ya utalii.

Mwenye kiti wa chama cha kitalii eneo hili la Pwani Victor Shitaka amesema tayari watalii hasa kutoka mataifa ya kigeni waliokua wamepanga kuadhimisha sherehe ya pasaka humu nchini wameanza kurejea makwao.

Shitaka ameongeza kuwa Kufikia sasa asilimia 30 ya watalii wakutoka humu nchini ambao walikua wamekodi hoteli za kitalii pia wameondoka.

Mwenyekiti huyo vile vile maedokeza kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watalii waliokua wamepanga kuzuru hoteli hizo  wakati wa pasaka wamefutilia mbali likizo zao.

Shitaka amesema kwamba huenda wakalazimika kuwatuma likizo ya lazima baadhi ya wafanyikazi wao huku wengine wapunguziwe mishahara.