Habari

WAKAAZI KWALE WALILIA FIDIA.

Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza ameitaka serikali ya kaunti ya Kwale kuwafidia wakaazi watakaoathirika na mradi wa kiwanda cha matunda katika eneo la Mathare huko Shimba Hills.

Akizungumza huko mjini Kwale, Tandaza amepinga vikali hatua ya wakaazi hao kufurushwa katika eneo hilo bila kulipwa fidia.

Mbunge huyo amewataka waathiriwa wa mradi huo wa serikali ya kaunti kutendewa haki ya ardhi yao.

Haya yanajiri baada ya familia 15 kutoka eneo hilo zikihofia kufurushwa katika ardhi hiyo ya serikali ya ekari 25 ili kutoa nafasi kwa upanuzi wa kiwanda hicho.

Hata hivyo, afisa mkuu katika wizara ya ardhi kaunti ya Kwale Nuru Mohammed amesema hakuna mkaazi atayefurushwa katika ardhi hiyo.