AfyaHabari

Wakazi Kwale Wahimizwa kuzingatia masharti ya Covid 19.

Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza amewaonya wakaazi wa kaunti ya Kwale dhidi ya kushiriki katika hafla za harusi na mazishi wakati huu ambapo kuna tishio la janga la corona.

Mbunge huyo amesema hafla hizo zimekuwa tishio kwa afya ya wakaazi ambao amewataka wazingatie kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Tandaza amewataka wakaazi kutilia maanani idadi ya watu wanaofaa kuhudhuria hafla hizo kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya corona nchini.

Aidha, Tandaza amewaomba wakaazi wa Kwale kuzingatia maagizo ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona hasa uvaaji wa barakoa katika sehemu za umma.

Mwisho