AfyaHabari

WAUGUZI TAITA TAVETA KUWASILISHA RUFAA KATIKA BODI YA UAJIRI KAUNTI HIYO.

Wauguzi walioshiriki mgomo kaunti ya taita taveta wana saa 48 kuanzia leo kuwasilisha rufaa katika bodi ya uajiri kaunti hiyo.

Hii ni baada ya maafikiano yaliyojiri kufuatia kikao baina ya wizara ya afya ya kaunti, bodi ya uajiri kaunti hiyo na muungano wa wauguzi.

Wanachama wao wamedokeza kuhusu maafikiano yao yakijumuisha usitishwaji wa agizo la kufurushwa katika makaazi yao ya kaunti hasa kwa wauguzi walioshiriki mgomo, kubuniwa jopo maalum kuangazia matakwa yao miongoni mwa mengine.