HabariSiasa

Karisa Nzai awakosoa baadhi ya wabunge kutokana na hamu ya serikali kukopa zaidi…

Mwaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la jomvu Karisa Nzai amekosoa baadhi ya wabunge kutokana na hamu ya serikali ya kukopa mikopo akisema kuwa wao ndio wanaochangia pakubwa katika mikopo hiyo.

Akizungumza katika kipindi cha sauti asubuhi hii leo, Nzai amesema baadhi ya wabunge nchini  wamejisahau katika kutekeleza majumu yao kikamilifu, huku wakiwahada wananchi, aidha anasema kwamba kutokana na tamaa  ya wabunge hao wakenya wa kawaida kwa sasa wanapitia hali duni ya maisha ikizingatiwa kwamba hali ya uchumi imedorora kwa kiasi kikubwa.

Kadhalaika kiongozi huyo amesema kwamba uongozi duni unaoshuhudiwa kutoka kwa baadhi ya viongozi nchini, umesababisha ukosefu wa ajira na hata chakula.