Watu 15 wamethibitishwa kuaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabani maeneo ya Kizingo kwenye barabara kuu ya Malindi Mombasa iliyotokea mwendo wa saa moja leo asubuhi.
Akithibutisha kisa hicho kamishna wa kaunti hiyo Kutswa Olaka amesema ajali hiyo imetokea baada ya basi la kampuni ya Muhusin lililokuwa limetokea Mombasa kugongana ana kwa ana na basi dogo la kampuni ya Sabaki Shuttle baada tairi kupasuka.
Olaka vile vile ameitaka kampuni inayorekebisha barabara hiyo kuharakisha ujenzi huo akisema huenda mitaro iliyoachwa wazi imechangia kwenye ajali hiyo.
Wakati uohuo kamanda wa Polisi kaunti hiyo Nelson Taliti amewataka madereva kuwa waangalifu barabarani ili kuzuia viasa kama hivyo akiwaonya wakaazi dhidi ya kuchukua nafasi hiyo kupora mali ya manusura.
Taliti amewashauri wakaazi kujitokeza na kutoa msaada kwa maafisa wanaojitokeza katika uokozi badala ya badala ya kutatiza uokozi.
Miili ya walioaga dunia imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya kaunti ndogo ya Malindi huku manusura wakikimbiza katika hospitali mbali mbali eneo hilo.