HabariMombasa

Familia zilizopoteza wapendwa wao zaendelea kuomboleza huko Kilifi…..

Baadhi ya familia kutoka eneo la Masaba kaunti ya Kilifi zinaendelea kuomboleza vifo vya wapenda wao waliofariki mapema hapo jana kufuatia ajali iliyotokea eneo la kwamkikuyu-Kizingo katika barabara kuu ya Malindi Mombasa.

Miongoni mwa familia hizo ni ambayo mpendwa wao alifariki dunia alipokuwa akitibiwa katika chumba cha matibabu ya dharura hospitalini.

Wamewataja wapendwa wao kama waliowategemea pakubwa katika familia zao.

Jumla ya watu 15 walifariki dunia kufuatia ajali hiyo, iliyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya Muhsin na Sabaki.

Haya yanajiri huku madereva wa mabasi na matatu zinazotumia barabara kuu ya Mombasa – Malindi sasa wakiitaka serikali kuharakisha ukarabati wa barabara hiyo wakisema imejaa mashimo na inahataraisha usafiri.

Baadhi ya madereva hao wanasema barabara hiyo ni nyembamba na inapaswa kupanuliwa ili kuwa rahisi kwa magari kupishana.

Wanasema ajali iliyotokea hapo jana imewashutusha mno huku wakihofia kazi zao.