Habari

Mwanaharakati Edwin Kiama aachiliwa kwa dhamana…………….

Mwanaharakati Edwin Mutemi Kiama aliyekamatwa kwa madai ya kusambaza bango la rais Uhuru Kenyatta ameachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu Shilingi 500,000 akisubiri uchunguzi kukamilika.

Polisi walikuwa wameomba siku 14 kuendelea kumzuilia Edwin Mutemi Kiama ili wakamilishe uchunguzi.

Lakini hakimu Mkazi mwandamizi wa mahakama ya Milimani Jane Kamau leo alikataa ombi la upande wa mashtaka, akisema hakuna sababu za kutosha zilizowasilishwa mbele ya mahakama kuidhinisha kuzuiliwa kwa mshukiwa.

Ameagiza Kiama kuweka mahakamani dhamana ya Shilingi laki tano pesa taslimu na aripoti kwa afisa wa uchunguzi kila siku kwa siku kumi.

Ameamuru kesi hiyo kutajwa mnamo Aprili 17, kwa maagizo zaidi.