Habari

Atwoli achaguliwa tena kuwa katibu mkuu wa COTU…

Katibu mkuu wa muungano wa  vyama vya wafanyikazi  nchini COTU Franscis Atwoli amechaguliwa tena kuhudumu katika wadhfa huo kwa miaka mingine  mitano.

Atwoli amechaguliwa bila kupingwa wakati wa shughuli iliyofanyika leo hii katika chuo kikuu cha tom mboya mjini Kisumu na kuhudhuriwa na wajumbe mia mbili hamsini.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa rasmi Atwoli ameishauri kutumia mikopo iliyopewa na shirika la fedha dunuani IMF kuwasaidia walioathirika na maambukizi ya corona nchini.

Atwoli amesema kuna haja ya kuwa na uwazi zaidi wa matumizi ya mikopo hio kwa kuwa  maambukizi ya virusi vya korona yameathiri maisha ya wakenya wengi nchini.

Hii ni mara ya tano kwa Atwoli kuchaguliwa katika nafasi hiyo mara ya kwanza alichaguliwa mwaka 2001 baada  Joseph Mghala.

Atwoli amewashkuru wafanyikazi wote akisema ataendelea kuwahudumia bila ubaguzi.