AfyaHabari

Watu 1,091 wapatikana na corona, huku 17 wakiaga dunia…….

Kenya hii leo imerekodi visa vipya 1,091 vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 7,300 zilizofanyiwa vipimo chini ya saa 24 zilizopita.

 

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 144,154 vya maambukizi ya corona.

 

Katika visa hivi vipya, 1,058 ni wakenya huku 33 wakiwa raia wa kigeni, 610 ni wanaume huku 481 wakiwa wanawake.

 

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

 

Hii leo watu 17 wamefariki dunia kutokana na maambukizi na kufikisha idadi ya watu waliofariki kutoka na corona kuwa 2,309.

 

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 533 wamepona virusi vya corona, 297 wamepona wakiwa nyumbani huku 236 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya waliopona kuwa watu elfu 98,183.

 

Jumla ya wagonjwa 1,605 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,233 wakiuguzwa nyumbani.

 

Wagonjwa 236 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).