BurudaniEntertainmentHabariMombasa

LAVIDOH:WALINIAMBIA SITAWEZA MZIKI………..

Lavidoh ni msanii mwenye uwezo wa kipekee kutoka hapa pwani ambaye kwa sasa anatamba ni kibao ‘Watanyooka’ chini ya Uongozi  wa Babaz Entertainment & Co, inayoongozwa na Ali Athman Mwambaya Almaarufu BABAZ. Lavidoh alipata umaarufu kupitia wimbo unaitwa Conifella amabao ulifanya vizuri kwenye chat Za Radio, mitaani na Kwenye Mitandao ya Kijamii. Uwezo wake umempa nafasi ya kipeke kwenye tasnia ya mziki, uwezo ulishawishi Marapa Reagani Dandy na Tricks Wote kutoka Kilifi na kumshirikisha kwenye Collabo yao inayotesa kwa sasa ‘KILIFI’

Kwenye mahojiano ndani ya Sauti Ya Pwani Fm msanii Lavidoh alifunguka na kusema kwamba Safari yake ya mziki haijakuwa rahisi hivyo kwani kuna baadhi ya watu waliwahi kumuambia hawezi kutoboa kimziki.