Habari

Wizara ya afya Taita yatakiwa kuweka kituo cha afya katika maeneo ya uchimbaji madini….

Changamoto imetolewa kwa wizara ya afya kaunti ya Taita Taveta kuweka kituo maalum cha afya katika maeneo ambako shughuli za uchimbaji madini zinaendeshwa.

Kulingana na washikadau wa madini, idadi ya juu ya watu katika maeneo ya uchimbaji  madini lazima iwe na huduma za afya kutokana na hatari ilioko maeneo hayo.

Haya yanajiri huku pia wakisema watoto wasiruhusiwe katika maeneo hayo ya uchimbaji madini kwani sio salama kwao.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,