AfyaHabariMazingira

Kamati ya afya Mombasa yatembelea daraja la liwatoni kutathmini hali…

Kamati ya afya katika bunge la kaunti ya Mombasa imelitembelea daraja la kuelea katika eneo la Liwatoni kutathmini kuhusu msongamano wa watumizi wa daraja hilo.

Hii ni baada ya hoja kuwasilishwa na mwakilishi wa wadi ya Bofu Ahmed Salama kuhusiana na msongamano huo ambao unahofiwa kuleta msambao wa virusi vya corona.

Salama alitaka kujua je hakuna hatari ya maambukizi ya virusi hivyo kwa kuwa abiria wote wametakiwa kutumia daraja hilo nyakati za asubuhi na jioni pia kutaka kujua aliyetoa agizo hilo bila kutaathmini msongamano.

Kamati hio inayoongozwa na mwakilishi wadi wa Miritini Kibwana Swaehe inatazamiwa kuwasilisha ripoti hio bungeni juma lijalo.