Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa wazi nafasi 4 katika tume ya uchaguzi nchini IEBC.
Katika gazeti rasmi la serikali Rais Kenyatta amewaalika watu kutuma maombi ili kufanyiwa mchujo wa kuwa makamishna wa tume ya IEBC.
Tangazo hilo linakuja wakati ambapo IEBC imeanza mikakati ya ununuzi wa vifaa vya uchaguzi wa mwaka wa 2022.
Nafasi hizo zilikuwa wazi baada ya makamishina Conslatan Kathamine na Margaret Mwachonya kujiondoa katika IEBC Aprili tarehe 16 baada ya mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati kutangaza kumwachisha kazi aliyekuwa afisa mkuu mtendaji Ezra Chiloba.
Kamisha wa kwanza kujiuzulu alikuwa Roselyn Akombe kabla ya marudio ya uchaguzi kuu wa mwaka 2017.