Habari

Watahiniwa wa KCPE Kilifi wasema COVID 19 imeathiri matokeo yao…

Watahiniwa wa mtihani wa darasa la nane KCPE kaunti ya Kilifi  ambao walipokezwa matokea yao wanasema  changamoto za ugonjwa wa Corona zilichangia wao kupata matokeo ambayo hawakutarajia.

Kulingana na wanafunzi wa shule ya kibinafsi ya Mnarani Preparatory ,wanasema walipokuwa nyumba wakati wa likizo ndefu hawakupata muda mzuri wa kusoma.

Wakiongozwa na Victoria Katana ambaye alipata alama 407 na kuwa wa kwanza katika shule hiyo, wanasema walikuwa wamesahau mambo mengi ya shule wakati walipokuwa nyumbani.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shule hiyo Everline Ruto amesema baada ya kuchipuka kwa ugojwa wa Corona wanafunzi wengi walisahau kila kitu ambao walikuwa wamesoma .

Ruto aidha amesema licha ya wanafunzi kukaa nyumbani muda mrefu walishirikiana na walimu na kutia bidii kuandikisha matokea bora .

Matokeo ya mtihani wa KCPE yalitangazwa hapo jana ambao shule za umma ziliandikisha matokeo bora huku mwanafunzi bora akiwa Faith Mumo kutoka shule ya msingi ya Kari Mwailu kaunti ya Machakos.